YAPATE HAYA SODO LA KITAA LA EBONY FM.


 

Pazia la michuano ya kuwania Mbuzi kule Iyayi  inaanza rasmi kesho kwa mchezo kati ya Kihowa Rangers na Mbilili.
Taarifa na Joseph Mhanzi.
………………………..
Kutoka Nyororo timu Nyroro Stars inawopongeza wachezaji wake kwa kuanza mazoezi vizuri.
Taarifa na Njiti Mavika aka Sendeu.
………………………..
Kwenye uwanja wa Ilembula  hii leo kulikuwa na mchezo kati ya Wapaliala na Utiga uliomalizika kwa sare ya bila ya kufungana.
Taarifa na Dalali Ilembula
……………………..

Katika kata ya usuka ligi imeendelea hii leo kwenye uwanja wa Lugoda kwa mchezo kati ya Usuka na Ikwega ambapo Usuka imeifunga Ukwega magoli 2 kwa 0.

Taarifa na Dalali Ilembula.
……………………
Moro cup kule Makambako timu ya Makambako Kids imeifunga Young Boys magoli 5 kwa 1
Na kesho ni mapumziko
Taarifa na mratibu wa michuanp Mr Moro.













0 comments:

Post a Comment