
Iker Cassilas
Nahodha wa timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas amekiri kuwa mchezo wa usiku wa jana dhidi ya Crotia ulikuwa mgumu sana kwao tangu kuanza mashindano hayo.
Katika matokeo ya goli moja kwa sifuri lilifungwa na Jisus Navas kwenye dakika ya 88 Casillas amesema kikosi chao hakikucheza vizuri ukilinganisha na michezo miwili iliyopita.
Aidha Cassilas amesema mbali na uwezo mdogo anaamini kikosi chao kitafanya vizuri kwenye hatua zinazofuta istoshe kutwaa ubingwa wa ulaya mwaka huu.
Kwa upande wake kiungo mshambuliaji wa Hispania,Andres Iniesta amekiri kuwa timu yao ilielemewa na kikosi cha Croatia kilicho ongozwa na vijana wenye uwezo wa hali ya juu.
Hispania ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo huku wakitazamwa kufanya vizuri kulinga na uwezo wawachezaji waliomo kwenye kikisi hicho
0 comments:
Post a Comment