RT YATOA MACHO KWA VIJANA.


                       
                        Katibu wa RT Suleymani Nyambui.
Uongozi wa shirikisho la riadha nchini RT, umetangaza dhamira ya kutumia michezo ya UMISETA inayoendelea mkoani Pwani kama chagizo la kuwapata wachezaji wenye umri mdogo ambao huenda wakawa watetezi wazuri wa Tanzania katika nyanja ya kimataifa siku za usoni.

Katibu mkuu wa RT Suleyman Nyambui amesema wamekua wakifuatilia michezo hiyo kwa ukaribu na wamebaini kuna vipaji vya hali ya juu ambavyo vinahitaji usaidizi wa kuendelezwa kwa ajili ya kufanya vyema kimataifa.

Baada ya manguli wa zamani wa riadha nchini akina Filbert Bayi na Suleimani Nyambui mpaka mchezo huo umekuwa chini kitaifa.

Je kwako msomaji wa Blogu hii tufanyaje?

0 comments:

Post a Comment