DROGBA ATUA SHANGHAI SHENUA

            
                                         Didier Drogba
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba hii leo amehamia rasmi klabu ya  Shanghai Shenhua ya China kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Mshambuliaji huyo amechezea klabu ya Chelsea kwa mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa taji la ligi ya mabingwa mwezi May mwaka huu ni hivi sasa anapata fursa ya kucheza na mshambuliaji mwenzake wa zamani Nikolas Anelka.
Mwamba huyo wa Ivory Coast atakumbukwa kwa bao alilofungia Chalsea walipocheza na Bayern Munich ya Ujerumani.Bao hilo liliifanya Chalsea ijiandikie historia ya kushinda kombe la Klabu bingwa bara Ulaya.
Drogba mwenye umri wa miaka 34 amesema kabla ya kuamua kuhamia China alifikiria kwa makin sana huku akisema kuwa ameridhishwa na uamuzi huo mbali na kupata mialiko mingi toka katika timu mbalimbali barani ulaya..
Drogba alijiunga na Chalsea mwaka wa 2004 kutoka Olympic Marseille ya Ufaransa kwa pauni million 24. Alikuwa baadhi ya wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Meneja Jose Mourinho alipojiunga na Chalsea.
Akiwa Chalsea kwa kipindi cha miaka minane, Drgoba aliisaidia klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu ya Uingereza mara tatu na kombe la FA mara nne.
Drogba anaondoka Chalsea akiwa ameandikisha historia ya kuifungia timu hiyo jumla ya magoli 157 hivyo kuwa mchezaji nambari nne katika kwa ufungaji wa magoli katika historia ya Chalsea.
Katika kujiunga kwake na timu hiyo ya Shanghai Shenhua , Drogba anasema jukumu lake la kwanza ni kufanya soka ya China itambulike duniani kote na kulitoa katika sura ya sasa ya soka hilo.

0 comments:

Post a Comment