ROONY KUWEPO UWANJANI KWA MARA YA KWANZA.



                                   
Katika kuelekea safari ya michuano ya ulaya hatua ya mwisho katika makundi ambapo leo ni mchezo wa kundi D kati ya England naUkrain tunaona yafuatayo Wayne Rooney anajipanga kuanza mchezo wake wa kwanza baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa michezo miwili na uefa.
Mbali na hilo England ina point nne kwenye kundu lake huku ikihitaji sare ama ushundi kwenye mchezo wa leo na iweze kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali wakati Ukraine inalazimika kushinda mchezo wa leo ili iweze kufufua matumaini ya kusonga mbele.
Lakini kuna mshambuliaji Andy Carrol huenda akaanza kwenye mchezo huo huku Roy Hogson akionekana kutazama zaidi kwa Dan Welbeck na Wyne Roony kuanza pamoja katika mchezo wa leo.
Hii inaleta shaka kwa kuwa Carrol alifanya makubwa kwenye mchezo wa awali dhidi ya Sweden ambapo alifunga goli la kwanza katika ushindi wa magoli 3 kwa 2 huku matumaini yaki hamia kwa Roony ambaye anarekodi ya kucheza michezo 74 na magoli28 ya timu ya taifa.
Carrol amesema anafikiri kufanya maandalizi binafsi ili kujiimarishia nafasi yake kwenye kikosi hicho cha simba wa tatu.
Kiukweli Roony ni nyota mahiri na yupo katika kiwango bora cha kimchezo na anahitajika sana kwenye kikosi cha England hayo ni Carrol.

0 comments:

Post a Comment