PAULE AMESEMA HAYA BAADA YA KICHAPO CHA JANA.


                             
Baada ya timu yake kutolewa na Hispania katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya kocha wa Ureno Paulo Bento amesema licha ya kupoteza pambano hilo  anamini hiyo ni hali ya kawaida kutokea katika soka.
Bento mwenye umri wa miaka arobaini na tatu amesema hawakuwa na bahati kwani katika muda wa dakika tisini vijana wake walicheza soka safi tofauti na muda wa nyongeza kabla ya kufikia hatua ya changamoto ya mikwaju ya Penalti.
Kwa upande wake nyota wa Ureno Joao Pereira amesema wamesikitishwa na matokeo hayo ambayo hawakutarajia kuyapata nakuongeza kuwa anaamini bahati haikuwa kwao kwani walijaribu kucheza soka safi.
Aidha mchezaji huyo amewashukuru mashabiki wa Ureno kwa kuwaunga mkono kuanzia mwanzo hadi usiku wa kuamkia leo walipotolewa na Hispania kwa penalti 4 dhidi ya 2 walizopata wao.

0 comments:

Post a Comment