YANGA PAWAKA MOTO KABLA YA UCHAGUZI


 
                                Ibrahim Akilimali
Kamati ya Baraza la wazee wa Yanga imemchimba mkwara mwanachama  Abeid Falcon kuwa watamuadhibu kutokana na kuweka pingamizi kwa wagombea wote wa wanaowania nafasi ya uongozi zilizoachwa wazi.

Akizungumza na Ebon Fm,  Katibu wa kamati hiyo Ibrahim Akilimali amesema Abeid anataka kuwachanganya wanayanga huku akisema yeye ni nani hadi awazibie wenzake haki ya kugombea.

Akilimali amesema ni lazima kanuni za katiba zifuatwe ndani ya klabu hiyo na mtu ambaye afuati katiba na kuingiza vitu vyake basi atafutwa uanachama kama kanuni zinavyosema.
 
 
                                     Bakili Makele
KWA upande mwingine Mwenyekiti wa vijana wa Yanga bakili Makele amesema kuwa kuna baadhi ya wanachama wanatumika kuiharibu Yanga huku akilenga kwa alikuwa mtangazaji wa kituo cha Channel ten Sprian Musiba kuwa  kuwa atulie na afanye mambo mengine au kuungana na wana Yanga ili kujenga Yanga mpya.

0 comments:

Post a Comment