STARS YAWASILI MSUMBIJI.


 
                                     Kikosi cha Stars
Tayari timu ya taifa ya Tanzania, TaifaStars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.

Stars yenye kikosi cha wachezaji 20 chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen imefikia Hotel 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa
Taifa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 10
kamili.

Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo
itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.

0 comments:

Post a Comment