NDOLANGA KUSHITAKI HABARI.


 
                                       Ndolanga.
Baada ya aliekua mwenyekiti wa chama cha soka nchini FAT kwa sasa TFF, Muhidin Ndolanga kutangaza kuifikisha mahakamani kampuni ya Habari Cooperation kupitia magazeti ya Mtanzania na Dimba.

Ndolanga ametangaza maamuzi hayo, kufautia madai ya kuchafuliwa na magazeti hayo kuwa yeye alinusurika kupigwa katika katika msikiti wa Kichangani.

Aidha amesema analazimika kufanya hivyo kufuatia vyombo hivyo kuendelea kumsema vibaya.

Hivi karibuni Ndolanga aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya msikiti wa kichangani huku ikiwa tayari ana cheo  cha uraisi wa heshima alichopewa mwezi wane mwaka huu katika mkutano mkuu wa TFF.

0 comments:

Post a Comment