Klabu ya AC Milan ya Italia imethibitisha kuwa kiungo wake raia wa Ghana Sulley Muntari atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji wa jereha la goti linalomsumbua.
Muntari anayesumbuliwa na tatizo la goti la mguu wake wakushoto siku ya jumanne ya wiki hii alipelekwa katika hospitali ya La Madonnina iliyopo jijini Milan nchini Italia kwa uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa daktari wa nyota huyo amesema kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji Muntari atachukua kipindi chamiezi mitano hadi sita kupona ili kurudi uwanjani.
Muntari alijiunga na AC Milan kwa mkopo msimu uliopita akitokea Inter Milan nakuonyesha uwezo mkubwa huku taarifa za ndani ya klabu yake ya sasa zilibainisha uwepo wa mipango ya kumsajili mmoja kwa mmoja msimu huu.
0 comments:
Post a Comment