
Siku chache baada ya shirikisho la soka la nchini Misri kuitaka timu ya taifa ya vijana ya Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki na timu yao ya vijana uongozi wa TFF umeibuka na yake.
TFF imetoa mashrti mazito kwa EFA kwamba mechi hizo zichezwe Julai 3 na Julai 5 mwaka huu kwa masharti maalumu. Ikiwa zitachezwa Misri, mwenyeji (EFA) atagharamia Ngorongoro Heroes kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya kufanyia mazoezi.
Kwa upande mwingine Angetile amesema maandalizi yako vizuri kwaajili ya Ngorongoro kushiriki michezo hiyo ya kirafiki
0 comments:
Post a Comment