MIICHUANO YA COPA COCA COLA HUENDA IKAINGIA DOSARI.


 
                Mvela kulia akiwa katika moja shughuli za soka
Zikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa mashindano ya Copa coca cola dalili za dosari zimeanza kukisiwa kujitokeza toka kwa wa andaaji wa mashindano hayo.
Katibu wa IRFA na Mjumbe wa kamati ya utendaji wa TFF Eliud Mvela amesema mpaka sasa hakuna kiasi chochote kilitolewa na waandaaji kwaajili ya nauli ya timu za mikoani.
Akizungumzia hilo sambamba na maandalizi ya timu ya vijana ya mkoa wa Iringa katibu wa IRFA Eliud Mvela amesema kwamba maandalizi ya timu ya Iringa yanakwenda vizuri na michezo ya kirafiki inaendelea kuchezwa.

0 comments:

Post a Comment