MWANZA YATOLEWA NJE KIAINA KAGAME CUP.

 
 Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza.
Siku moja baada ya kupata malalamiko ya viongozi wa soka  mkoa wa mwanza Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini TFF Angetile Osiah amewataka viongozi wa soka mkoani humo   kugharamia usafiri wa timu shiriki katika michuano ya kagame ili michuano ifanyike katika mkoa huo.

Shirikisho la soka nchini TFF limekitaka chama cha soka cha jiji la Mwanza kugharamia gharama za usafiri wa timu shiriki za michuano ya Kagame inayotaraji kuanza julai 14 mwaka.

Mkoa wa Mwanza uliomba kuwa moja kati ya miji itayotumika kwa michuano hiyo mikubwa Afrika Mashariki na kati.

Katika maelezo ya awali ya TFF kupitia katibu wake mkuu Angetile Oseah amesema kuwa ni vigumu kusambaza mashindano hayo katika kila mkoa kutokana na ukata uliopo na mashindano hayo kukosa udhamini huku akitoa mfano kuwa mwaka uliopita michuano hiyo ilikwenda Morogoro kwa gharama za Mdhamini huku wakizingatia umbali wa eneo husika.

0 comments:

Post a Comment