MIKI ROQUE AFARIKI DUNIA


 
Mlinzi wa kutumainiwa wa klabu ya Real Betis ya Hispania Miki Roque mwenye umri wa miaka ishirini na tatu amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa.
Habari zilizothibitishwa na vyombo vya habari nchini Hispania zimesema mchezaji huyo aliewahi kuichezea timu ya taifa hilo kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi na tisa alibainika kuwa na ugonjwa huo mwaka jana kufuatia vipimo alivyofanyiwa.
Imeelezwa kuwa mara baada ya kukutwa na tatizo hilo klabu yake ilijitahidi kumpatia matibabu bila mafanikio hadi kifo kilipo mkuta.
Katika maisha yake ya soka amewahi kuichezea Liverpool ya England kati ya mwaka 2005 hadi 2009  kabla ya kuhamia Real Betis msimu wa 2010 na 2011 kabla ya kuacha kucheza  soka baada ya kupatwa na maradhi ya kansa yaliyochukua maisha yake.

0 comments:

Post a Comment