
Hii huenda ikawa sawa na kauli ya mkataaa kwao mtumwa watu wengi wanafahamu kama sehemu kubwa ya maisha ya mshambuliaji wa Argentina Leon Mess ni Hispania sasa leo kiungo huyo ameibuka na haya.
Amesema angependa kuona timu ya taifa ya Hispania ikitwaa taji hilo ndani ya mwaka huu wa 2012 huku katika taarifa yake hiyo akiwaorodhesha majembe ya timu yake Andres Iniesta , Xavi Alnandez na miamba mingine kuwa itakuwa poa kama watatwaa ubingwa msimu huu.
Messi amesema kuwa anakiri kukosa haki ya kushiriki michuano hiyo ya Ulaya ila anapenda kuona Spain inatwaa ubingwa ulaya.
Hispani iliyokuwa ikitokea kundiC haijafungwa hata mchezo mmoja mpaka sasa mbali na ule waliomaliza kwa sare dhidi ya Italia huku ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo kutokana na aina ya soka wanalocheza.
0 comments:
Post a Comment