HASHIM ATAKA TBF IANDAE MIPANGO THABIT


                     
Hii leo Mchezaji wa kimataifa wa mpira wa kikapu Hashim Thabiti amelitaka Shirikisho la mchezo huo nchini TBF kuandaa mipango maalum ya kuinua vipaji vya vijana hapa Tanzania.

Hashimu amesema kuwa kuna vijana wengi wana vipaji vya kuchezo mchezo huo isipokuwa hawana vyanzo vya kujiendeleza kwa mchezo huo.

Mwana kikapu huyo anayecheza kikapu kule nchini Marekani akiwa katika harakati zake za kuandaa vijana bora wa kikapu amesema elimu pia inapewa nafasi kubwa katika mchezo huo kwa hiyo ni jukumu la wazazi kuhamasisha watoto wazingatie pande zote.

0 comments:

Post a Comment