VAN MARWIJK ATIMULIWA KAZI


               
Siku kadhaa baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya kombe la mataifa ya Ulaya huko Poland na Ukrain hatimae shirikisho la soka nchini Uholanzi limekatisha mkataba na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa hilo Bert Van Marwijk.
Katika kikao kilichofanyika baina ya kocha huyo na shirikisho hilo pande hizo mbili zikekubaliana kukatisha mkataba uliokuwa unamalizika hadi mwaka 2016.
Baada ya kufikia uamuzi huo mkurugenzi wa shirikisho hilo Bert Van Oostveen amesema wanamshukuru kocha huyo kwani tangu wawe naye ameliwezesha taifa hilo kufanya vizuri kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2010 kiasi chakushika nafasi za juu kwa ubora wa soka duniani.
Marwijk mwenye umri wa miaka sitini alishika hatamu ya kuifundisha Uholanzi mwaka 2008 baada ya aliyekuwa kocha kipindi hicho Marco van Basten.

0 comments:

Post a Comment