PRANDELLI AKIPONGEZA KIKOSI.


 
                        Kocha wa Italia,Cesare Prandelli
kocha wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli amekisifu kikosi chake kwa ushindi wa penati nne kwa mbili uliopatikana jana dhidi ya England.
Prandelli amesema kikosi chake kimefanya kinachostahiki kufanywa licha ya kukosa nafasi nyingi za kufunga huku akikiri kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu sana kwake.
Aidha amesema kwa sasa akili na mawazo yote yanalekezwa katika mchezo wa  nusu fainali utakaochezwa  juni 28 kwenye uwanja wa Narodow uliopo nchini Poland.
Mbali na mchezo huo nusu fainali nyingine itachezwa Juni 27 kwenye uwanja Dombas Arena kule Ukrain ambapo Ureno itacheza na Hispania.

0 comments:

Post a Comment