BENITEZ AONESHWA NJIA NYINGINE NCHINI ITALIA.


            
Kocha wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez yupo njiani kutwaa kibarua katika klabu ya Sampodoria ya nchini Italia.
Hayo yamethibitishwa na mmliki wa klabu ya Sampodoria Ricardo Garone kuwa wapo kwenye mazungumzo na kocha wa huyo kihispania na wakati wowote watakamilisha suala la kazi yake.
Garone ameongeza kuwa Benitezi anavutiwa kwa kiasi kikubwa na kikosi cha Sampodori tangu timu hiyo inashiriki Serea B kabla ya kurejea katika  nafasi yake ligi kuu ya nchini Italia Serea A.
Maelezo hayo pia yametokana na kocha wa timu hiyo Lanchini Beppe aliposema kuwa Benitez anampango wa kujiunga Genoa nasi Sampodoria.

0 comments:

Post a Comment