BARTON KILICHOMKUTA NI HIKI NDANI YA QPR.


         
            Barton akiwa katika moja ya vurugu zake.
Kiungo wa klabu ya QPR Joey Barton amevuliwa unahodha wa klabu hiyo pamoja na kupewa adhabu kubwa na uongozi wake wa QPR huku adhabu hizo zikielezwa kuwa zinatokana na vurugu za kizembe alizozifanya dhidi ya Manchester City.
Baada ya majadiliano makubwa kati ya Uongozi wa QPR na benchi la ufundi lilifikia hatua ya kumkata Barton kiasi cha paundi 430,000 ikiwa sawa na mshahara wake wa wiki sita huku akivuliwa rasmi unahodha wa timu hiyo.
Barton mwenye umri wa miaka 29 tayari amefungiwa takribani michezo 12 na shirikisho la soka la England FA kwa kosa la kuwabuguzi Carlos Tevez na Sergio Aguero katika mchezo wa mwisho wa ligi ya England.
Mbali na adhabu aliyopewa nyota huyo pia atakosa ziara ya klabu hiyo inayotaraji kwenda barani Asia kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Katika maisha yake ya soka Barton alizitumia timu za Manchester City na NewCastle united kabla ya kujiunga na QPR.

0 comments:

Post a Comment