
Alan Pardew
Siku mmoja baada ya kutangazwa kwa ratiba ya ligi kuu ya England kocha wa Newcastle United Alan Pardew amezungumzia mechi ya ufunguzi baina ya timu yake na klabu ya Totenharm itakaopigwa kwenye uwanja wa Sports Direct Arena.
Kocha huyo aliyeiwezesha Newcastle kung’ara msimu uliopita amesema anajisikia faraja kuanzia nyumbani kwa mara ya pili mfululizo ndani ya miaka miwili baada ya msimu uliopita kuanza ligi akiwa nyumbani dhidi ya Arsenal.
Amesema ni matarajio yao kuwa watashinda pambano hilo licha ya kwamba utakuwa mmoja kati ya michezo migumu kwao na kuwaahidi mashabiki wao kuwa hiyo itawasaidia kuanza vyema msimu mpya.
Ameongeza kuwa nia yao kubwa ni kufanya vyma msimu huu lakini kwa sasa akili yake ni namna atakavyoukabili mchezo wa kwanza dhidi ya Spurs ambayo hivi karibuni imekimbiwa na aliyekuwa kocha wake Harry Redknapp.
0 comments:
Post a Comment