
Mabingwa wa soka wa Uganda, Express FC, wanataraji kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la kagame, Dar es Salaam Young Afrika mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hapo kesho
Kocha msaidizi wa Express FC Charz Sayuku amesema kuwa wachezaji wake wana hali ya ushindi katika mchezo huo na ana uhakika wa kupata kipimo tosha cha kwa wachezaji wake kabla ya kuanza kwa michuano ya Kagame Cup.
Wakati huo huo mabingwa wa soka wa Tanzania, Simba SC, wanatarajiwa kucheza na mabingwa wa soka wa Uganda, Express FC, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopangwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, maandalizi yote kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika na kwamba kikosi cha Simba kitaundwa na wachezaji wapya na wa zamani
0 comments:
Post a Comment