Kagawa na kiongozi wa Man U akimaliza suala la uhamisho jana jioni
Klabu ya Manchester United imetangaza rasmi kumsajili kuingo wa Borussia Dotmund Shinji Kagawa kwa dau ambalo limewekwa kwenye mabano.
Hii imekuja baada ya mapema mwezi huu uongo wa Borussia na Man United kufikia muafaka wa kuuziana nyota huyo lakini leo usiku wa jana ulikuwa wenye mafanikio kwa united baada ya Kagawa kupita katika vipimo vya afya ikiwa na maana tayari ni mchezaji rasmi wa Manchester united
Kagwa kwa sasa anasubiri kukabidhiwa kibari cha kucheza ligi nchini England baada ya hapo ni kufanfa kazi na united kwa muda wa miaka minne kama mkataba wake unavyotaka na kuanza kufanya kazi julai 1 mwaka huu.

Kwa upande wa meneja wa timu Manchester united Sir Alex Ferguson amefarijishwa na kitendo Kagawa kujiunga na timu hiyo huku akiahidi makubwa katika kikosi chake cha msimu ujao.
Ferguson amesema Kagawa ni kijana mwenye umri wa miaka 23 na amefarijishwa kwa kitendo cha kiungo huyo mwenye ujuzi mkubwa wa soka kijiunga na timu yake.
0 comments:
Post a Comment