MBEYA KUPELEKA TIMU YA VIJANA KWA HALI YOYOTE.


Chama cha soka cha jijini Mbeya kimeahidi kufanya jitihada za dhati ili kusafirisha timu yao ya Copa coca cola hata nauli haijatolewa na waandaaji wa michuano hiyo ya vijana.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa FA Mbeya David Mwamaja huku akisema kuwa maandalizi ya timu yapo vizuri kwa kiasi kikubwa.
Amesema lengo la kupeleka timu kwenye mashindano inatokana na kuwa na dhamira kubwa ya kukuza soka la vijana.

Jiji la mbeya ndio jiji pekee lilitoa timu ya wanawake katika ile michuano ya airtel rising stara toka nyanda za juu kusini.

0 comments:

Post a Comment