KIKOSI kamili cha Simba SC kimewasili jijini Mwanza leo asubuhi tayari kwa ajili ya ziara yake ya kutembeza Kombe la Ligi Kuu ya Vodacom na kucheza mechi za kirafiki katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga imefafanua kuwa mamia ya wakazi wa Mwanza walijitokeza barabarani kuwalaki Wekundu wa Msimbazi katika tukio hilo la kihistoria kwa vile hakuna klabu iliyowahi kutembeza kombe kwa washabiki wake kama Simba mkoani hapa.
Baadhi ya washabiki hao walipata nafasi ya kuligusa kombe hilo na wengine walisikika wakipiga simu kwa ndugu na jamaa zao wakisema walau wamepata fursa ya kuligusa kombe hilo.
Simba imeleta kikosi chake kamili cha wachezaji wapya na wa zamani, ambacho kesho kitashuka uwanjani kucheza na Toto African (Wana Kishamapanda) katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini hapa.
Wachezaji wapya wa Simba kama vile Kanu Mbiyavanga, Paulo Ngalema, Abdallah Juma, Salim Kinje na Kigi Makassy wanatarajiwa kuvaa uzi mwekundu kwa mara ya kwanza katika mechi hizi za kanda ya ziwa.
Keshokutwa, Simba itacheza na mabingwa wa Uganda, Express, katika pambano litakalopigwa katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya ziara ya Simba katika mikoa ya kanda ya ziwa, John Kadutu, mabingwa hao wa Simba watatembeza kombe wakiwa na Simba mjini Shinyanga.
Wakati huo huo, KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, anatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airline) tayari kabisa kutekeleza programu yake ya mazoezi kwa ajili ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Wakati huo huo, KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, anatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airline) tayari kabisa kutekeleza programu yake ya mazoezi kwa ajili ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment