Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limekiadhibu chama cha soka cha England FA kiasi cha Euro elfu tano baada ya mashabiki wake kujaribu kuvamia uwanja kwenye mchezo dhidi ya Sweden katika kombe la mataifa ya Ulaya huko Poland na Ukrain.
Aidha Uefa imesema chama cha soka nchini Croatia HNS kinakabiliwa na adhabu kutokana na vitendo vya kinidhamu viwanjani vilivyofanywa na mashabiki wake kwenye mchezo dhidi ya Hispania uliochezwa jumatatu ya wiki hii.
Pamoja na mashabiki kusababisha adhabu hiyo wachezaji wa timu ya taifa ya Croatia wanachunguzwa baada ya kuonyeshwa kadi za njano takribani sita kwenye mchezo huo ambao Hispania ilishinda kwa taabu goli moja kwa sifuri.
Kamati ya nidhamu ya Uefa jumapili ya wiki hii inataraji kutangaza maamuzi juu ya tuhuma hizo.
0 comments:
Post a Comment