
Klabu ya Orlando Pirates inakaribia kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Uganda Emanuel Okwi huku kukiwa na uwezekano wa nyota huyo kujiunga Orlando wiki ijayo.
Kwa mujibu wa taaarifa toka nchini Afrika ya kusini kwamba Okwi huenda akajiunga na klabu hiyo bingwa ya Afrika ya kusini kwa dau la 680000.
Kabla ya msimu huu Okwi mwenye umri wa miaka 20 alikwenda Kaizer Chiefs na kufanya majaribio ya soka la kulipwa na kuondolewa baada ya kushindwa kuhudhuria jaribio la pili kwenye klabu hiyo.
Tayari Okwi alifungwa magoli mawili na kusababisha magoli matatu kwenye ushindi wa magoli 5 kwa 0 dhidi ya mahasimu wao Yanga ameweka doa la kucheza michezo takribani 17 ya timu ya taifa na kufunga magoli 11 ndani ya Uganda.
Mwaka 2010 alikuwa kinara wa kufunga magoli akiwa na kikosi cha Uganda katika michuano ya CECAFA akiwa na Uganda alipofunga manne katika mechi tano.
Ikumbukwe tu hivi karibuni Okwi alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa kigeni katika ligi kuu ya Tanzania bara katika zile tuzo chama cha waandishi wa habari za michezo Taswa.
0 comments:
Post a Comment