
Nyota wa klabu ya Sevilla inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispania Federic Kanout hatimaye ameweka bayana nia yake ya kuihama timu yake msimu huu wa Usajili.
Kanoute mwenye umri wa miaka thelathini na nne amesema hivi Karibuni alisafiri hadi China kufanya mazungumzo na mmoja ya klabu inayoshiriki ligi kuu ya huko CSL nakusistiza kuwa mazungumzo bado yanaendelea.
Amesema pamoja na kupokea maombi kutoka klabu mbalimbali, hivi karibuni atafanya chaguo sahihi ni wapi ataelekea nakubainisha kuwa anataraji kumaliza soka lake nchini China ama Marekani.
Tayari aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba amesha jiunga na klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China akiungana na mchezaji wa zamani wa Chelsea Nicolas Anelka.
0 comments:
Post a Comment