
Joachem Loew
Licha ya kikosi chake kufanya vyema kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya yanayoendelea nchini Poland na Ukrain kocha wa timu ya taifa ya Ujeruman Joachim Loew amesema kuwa bado timu yake haipo kwenye kiwango anachokitaka.
Mabingwa hao wa Ulaya kwa mwaka 1996 hadi sasa hawajafungwa mchezo hata mmoja kiasi cha wadadisi wa mambo kupigia chepuo kuwa huenda wakafikia fainali kama sio kutwaa kombe hilo kwamujibu wa kocha huyo licha ya kushinda jana dhidi ya Denmark amesema anahitaji kuimarika zaidi.
Pamoja na kukiri kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu amezungumzia eneo la ushambuliaji kuwa walipoteza umakini hususani kipindi cha kwanza kabla ya kubalika nusu ya pili ya mchezo huo.
Kutokana na ushindi wa jana Ujeruman itakutana na Ugiriki june 22 katika hatua ya robo fainali kwenye uwanja wa Baltic Arena unaochukua watazamaji wapatao elfu arobain na tatu mia sita kumi na tano.
0 comments:
Post a Comment