MKWASA AMWAGA MANYANGA HUKU AKIMPA ULAJI MDOGO WA GUMBO


                    
                                     Mkwasa akiwa kazini
Taarifa yenye kuaminika inasema kuwa kocha wa timu ya taifa ya soka la wanawake Tanzania Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu wadhifa kuinoa timu hiyo aliyokuwa akiino kwa Takribani miaka mine sasa.
Wakati akizungumza na www.drmuwa.blogspot.cpm Mkwasa amesema kuwa ameachia ngazi kwa nia njema na katika lengo la kujenga  timu hiyo kwa kuwapisha wengine washike nafasi yake.
Amesema ameshika timu kwa muda na ameona kwamba uwezo wake umeshafika kikomo katika kuinoa timu hiyo ya wanawake aliyowahi kuipeleka kwenye michuano ya Afrika mwaka 2010.
Aidha Mkwa amesema kwa sasa anaangalia zaidi kuipeleka timu yake ya Ruvu Shooting sehemu nzuri ya michuano ya ligi kuu bara.
Amezungumzia mchakato wa usajili huku akimtaja nyota chipukizi anayecheza katika kikosi chake cha pili Hassani Gumbo ambaye ni mdogo wa kiungo wa Yanga Rashidi Gumbo kuwa yumo katika Orodha ya nyota watakao tamba mwakani kwenye ligi kuu.

0 comments:

Post a Comment