Ezekiel Kamwaga
Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara wekundu wa msimbazi Simba wapo katika mchakato kabambe wa kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano mbalimbali.
Afisa habari simba Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wapo makini katika mashindano ya mwaka huu kwa kuwa wanawaona wapinzani wao wapo katika pilika za kusajili wachezaji wazuri.
Kamwaga amesema wapo imara kwa kila mashindano yaliyopo mbele yao na ana amini kuwa Kocha anaandaa kikosi vizuri huku akisisitiza kuwa ushindi na ubingwa ni jadi yao.
0 comments:
Post a Comment