
Washindi wa pili wa ligi kuu Tanzania bara, Azam FC wanajiandaa na Mashindano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) yanayoandaliwa na Baraza la Vyama ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yatafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-29 mwaka huu ambapo timu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya Juni 25 mwaka huu.
Akizungumza nami msemaji wa Azam Fc Jafari Idd Maganga amesema wapo tayari kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na msisimko wa hali ya juu.
Mbali na hilo Jafa amethibisha kuwa timu hiyo imesajili nyota wawili tu msimu huu akiwemo Dida wa Mtibwa na Odhiambo ama Blackbery kutoka nchini Kenya.
0 comments:
Post a Comment