
Andrey Shevchenko
Aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ukrain Andrey Shevchenko ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa lake baada ya kuingoza kwenye fainali za kombe la mataifa ya Ulaya zinazoendelea hivi sasa.
Shevchenko mwenye umri wa miaka thelathini na tano amesema atatumia mchezo mmoja tuu wa kirafiki utakaoihusisha timu yake ya taifa ili kuwaaga mashabiki wa timu hiyo.Juu ya timu yao kuondolewa kwenye fainali hizo na timu ya taifa ya England usiku wa jana nyota huyo amesema amejisikia huzuni kwakuwa ni miongoni mwa waandaaji huku akikubali matokeo na kusema kuwa katika soka lolote linaweza kutokea.
Shevchenko alizaliwa mwaka 1976 amecheza vilabu vitatu tofauti huku akiwa na rekodi ya kucheza 111 na kufunga magoli 48 .
0 comments:
Post a Comment