
Mashindano ya Copa coca cola yameendelea kushika kasi
Dodoma imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Juni 27 mwaka huu) kuifunga Mbeya mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha mkoani Pwani.
Mabao ya Dodoma katika mechi hiyo ya kundi C yalifungwa na Japhet Lunyungu dakika ya 59 wakati Frank Kaji aliwahakikishia ushindi washindi dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho baada ya kupachika bao la pili.
Nayo Mjini Magharibi iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Mmatokeo ya jioni hii ni haya.
Lindi 1Vs Ilala 0.
Manyara 2 vs Kaskazini Pemba 2.
Kinondoni 3 VS Mtwara 0.
Kusini Unguja 1 Vs Shinyanga 2.
0 comments:
Post a Comment