ZOFF AMEOTA NDOTO HIZI ZA KIHISTORIA.



Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Dino Zoff amesema taifa lake lina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ulaya msimu huu.

Zoff amesema hayo ikiwa ni siku mbili kabla ya kucheza na Ureno katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo ni hatua moja kwa Italia kufika fainali.

 
                              
                                                 Dino Zoff
Zoff mwenye umri wa miaka 70 aliwahi kutwaa taji hilo mwaka 1968 huku akisema kuwa mchezo huo utakumbusha michezo ya mwaka 1982 walipoifunga  ujerumani magoli 3 kwa1 kwenye fainali ya kombe la dunia nchini Hispania.

Mbali na mchezo huo nusu fainali ya kwanza itachezwa kesho kati ya Hispania na Ureno ambapo mpaka sasa Ureno inapewa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wake.

0 comments:

Post a Comment