Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Young Africans, John Mkwawa ametoa ufafanuzi wa dhana ya wagombea nafasi za uongozi wa klabu hiyo kusaidia shughuli za kifedha klabuni hapo, hatua mbayo inapokelewa kama rushwa kwa kushinikiza wanachama kuwapigia kura katika uchaguzi utakaofanyika July 15 mwaka huu.
Kiongozi huyo amesema dhana hiyo huenda ikawa na ukweli wa rushwa, lakini amewataka wanachama kutambua umuhimu wa kila mmoja ndani ya klabu hiyo linapokuja suala la kusaidia shughuli za kifedha.
Naye mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Deogratius Lyato amesema kamati hiyo ipo tayari kushirikiana na kamati ya klabu ya yanga endapo itatakiwa kufanya hivyo kufuatia kasoro zitakazojitokeza.
Wakati Lyato akisema hayo Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeendelea kumshangaa mwanachama wake Abeid Abeid Falcon kutoa pingamizi la kutoikubali kamati hiyo ilihali alishawania nafasi ya uongozi klabuni hapo.
0 comments:
Post a Comment