ROONY ARUDI VIZURI UWANJANI


 
Mshambuliaji wa Manchester united Wayne Rooney alikaribishwa kama shujaa katika timu ya England usiku wa jana, baada ya kutokuwepo kwa muda kufuatia adhabu ya UEFA, nasema hivyo kwa maana ya Roony kufunga bao pekee na la ushindi kwa timu yake dhidi ya Ukraine na kuifanya England kutinga robo fainali ikiwa kinara wa kundi D.
Krosi ya Steven Gerrald imemfanya Roony afunge goli katika dakika ya 48 ambapo goli hilo lilikuwa goli la uokozi kwa timu hiyo kutokutana na mabingwa watetezi Hispani na badala yake kucheza na Italia.
Lakini pia Ukraine walistahili kupata bao wakati mkwaju wa Marko Devic ilikuwa wazi umevuka mstari, lakini kufuatia juhudi za John Terry katika kuondosha mpira huo, pengine mwamuzi alishawishika kwamba kweli mpira haukuvuka msitari.
Ushindi wa Sweden wa magoli 2-0 dhidi ya Ufaransa ulihakikisha kwamba England wanafuzu kuingia robo fainali kama timu iliyoongoza katika kundi D.

0 comments:

Post a Comment