Kikosi cha Prisons ya Mbeya kilicho pandisha timu.
Kukiwa na wimbi kubwa kusajili nyota kwenye vilabu vya ligi kuu ya Tanzania bara klabu ya Tanzania Prisons imesema kuwa suala la usajili wanalikamisha ndani ya siku moja baada ya leo.
Wakati usajili wa ligi kuu bara ukiendelea na kule barani ulaya timu ya Tanzania Prisons imesema kuwa bado ipo katika harakati za usajili na inatarajia kumaliza ndani ya siku mbili hizi.
Katibu wa Tanzania Prisons Sadik Jumbe amesema kuwa wachezaji wao wapya watawatangaza kesho kutwa mara baada ya kufunga milango ya usajili.
Kwa upande wa kocha Tanzania Prisons imeajiri kocha mpya na kumfungisha virago Stefen Matata alieipandisha daraja timu hiyo lakini Jumbe amekataa kuzungumzia hilo wa kutaja jina la kocha mpya huku akidai kuwa ataweka bayana jina la kocha mpaka pale watakapo ingia mkataba na kocha huyo.
0 comments:
Post a Comment