HALI YA JANA ULAYA


                
                     Torres akishangilia bao usiku wa jana
Fainali za michuano ya ulaya zimeendelea jana kwa michezo miwili ya raundi ya pili hatua ya makundi katika kundi C.

Mchezo wa kwanza wa fainali hizo ulikutanisha timu za Italia na Crotia na kumaliza kwa sare ya goli 1 kwa 1 huku mchezo wa pili ukiinua timu ya Hispania baada ya kuitoa kafara Jamhuri ya Ireland kwa kuichapa magoli 4 kwa 0.

Aidha matokeo hayo yamebadili msimamo wa kundi hilo ambapo Hispania kwa sasa inaongoza kundi ikiwa na alama nne ikifuata timu ya Crotia nafasi ya pili wakati Italia ikishika nafasi ya tatu na Irelanda ikiwa ya nne.


Usiku wa leo tunakwenda kuangalia michezo miwili mikubwa wakati ya France wakicheza na Ukrain majira ya saa moja kamili huku saa 3:45 England wakiwa na kibarua kigumu juu ya timu ya Sweden.

0 comments:

Post a Comment