Raisi wa Vasco Dinamite
Rais wa klabu ya Vasco da Gama ya nchini Brazil Roberto Dinamite amesema timu yao haijapokea maombi kutoka kwa klabu ya Ac Milan juu ya kumsajili nyota wa klabu hiyo Ded.
Dinamite amesema kuwa kama Milan wanahitaji saini ya mlinzi huyo wa kibrazil hakuna budi kufika nchini Brazil kufanya mazungumzo ya mauzo ya mchezaji hiyo.
Lakini hakuweka wazi kama wapo tayari kumruhusu Dede anayetakiwa na Milan kama mbadala wa Thiago Silva aliyeripotiwa kukaribia kukamilisha taratibu za usajili wa kujiunga na PSG nchini Ufaransa.
Mbali na fununu za kutakiwa na miamba hao wa Italia Dede mwenye umri wa miaka 23 ametajwa pia kuwaniwa na mabingwa wa Serie A klabu ya Juventus turin.
0 comments:
Post a Comment