WILDE KUREJEA NCHINI MWAKANI.


              
Taarifa njema kwa watanzania kuwa Chris Wilde raia wa Marekani aliyekimbia kilometa 50 kuipa Tanzania zawadi ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ameahidi kurejea tena mwakani kukimbia kilometa 51 katika mbio za kutimiaza miaka 23 tangu kuanzishwa kwa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.
Wilde ambaye ni mganga msaidizi kutoka jimbo la Minnesota amekuwa mtu wa kwanza kukimbia kilometa 50 kusheherekea uhuru wa Tanganyika alipokimbia katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili tarehe 24 mjini Moshi.

Ikimbukumbwe mbio hizo zilifanyika kuanzia Moshi Club hadi Rau madukani na kurudi. Chris Wilde alirudi mara 9 na nusu ili kutimiza kilometa 50 kama zawadi kwa nchi ya Tanzania.

Akizungumza kabla ya kuondoka nchini Wilde alisema kuwa anaipenda sana Tanzania na ili kuidhihirishia dunia kuwa mlima Kilimanjaro uko Tanzania, amakimbia mbio za Kili kama zawadi kwa Tanzania.

Wakati Wilde akikimbia mbio  hizo siku yajumapili tarehe juni 24 aliongozana na mwanariadha wa kimataifa mtanzania Nelson Brighton na ambaye anakwenda nchini Marekani mwezi ujao kushiriki katika mbio mbalimbali zilizoandaliwa kwa ufadhili wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.

Chris Wilde aliungana na mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon na kuzifanya kuwa mbio zinazovutia washiriki wa Kimataifa. Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances kutoka Bethesda nchini Marekani.

Kumiminika kwa wakimbiaji wa Kimarekani, Ulaya, Australia, Canada na Scandinavia katika mbio za Mt. Kilimanjaro marathon ni neema kubwa kwa taifa hili ambalo lina hazina kubwa sana ya wanamichezo wanaotakiwa kuendelezwa.

Ni mbio zilizokwisha kupewa tuzo na majarida mbalimbali yanayoheshimika duniani kama vile Wonders of World ambalo lina wasomaji zaidi ya milioni 5 ambalo lilizipa nafasi ya pili wakati ambapo jarida linaloheshimika la Forbes lilizipa nafasi ya kwanza kama mbio zinazovutia.
Imetumwa na

WIZIRI MUKANGARA APATA AJALI.


            https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjBwhzCmahKPE6Ef0hbdkDq-AfmqCAjCTtiXDB2QD7bM20Q8ZN8WnfbnSaOg5w1FH71lKpBL0PYI9DdfX8kV_qwli-lxWeeQRBUNlk-scKgLTH1scP2gVjGSzG4WZQydgXgtjRiMdZQ-l4/s1600/Dk.+Fenella+Mukangara,+Waziri+wa+Habari,+Vijana,+Utamaduni+na+Michezo.JPG
Taarifa nzito ilizotufikia hii leo ianeleza kuwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara amepata ajali ya gari wakati akielekea jijini Mwanza leo.
Waziri Mukangara amepata ajali hiyo mkoani Tabora wakati akielekea jijini Mwanza kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Vishale maarufu kama Darts.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari imeenlezwa kuwa Gari la Waziri Mukangara limegongana na basi la Green Star na waziri huyo yupo hospitali ya mkoani Tabora kwa matibabu zaidi.
Lakini pia tunamshukuru mungu katika ajali hiyo hakuna mtu aliefariki.

DEIDRE LORENZ KULETA WACHEZA SINEMA NCHINI


 
Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.
Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana Tanzania.
“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote”aliendelea kusema Deidre Lorenz.
Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana.
Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental Races.
Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
Kwa kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.
“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.
Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.
Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.

YAKUBU AKIMBILIA CHINA.


 
Wimbi la wachezaji wakongwe wenye asili ya kiafrika kuhamia barani Asia linazidi kuongezeka baada Yakubu Ayegbeni kusaini katika klabu ya Gunzou ya nchini china.
Yakubu amesaini mkataba wa miaka mitatu na kuthibitisha kuikacha klabu ya Blackburn Rover alieitumia katika msimu wa 2011 na 2012.
Kwa upande wa klabu ya Ganzou, imekataa kubainisha thamani ya mkataba wa mchezaji huyo wa Nigeria alielitumikia taifa lake bila ya mafanikio tangu mwaka 2000.
Mpaka sasa wachezaji wengine wenye asili ya kiafrika wakiwemo Samuel Etoo, Didier Drogba pamoja na Mfaransa Nicolas Anelkawamemia vilabu vya barani Asia.

MAGOLI YA BAROTELI YAIPELEKA ITALY KOMBE LA MABARA.


          
Baada ya kikosi cha timu ya taifa ya Italia kuingia fainali ya michuano ya ulaya shirikisho la soka duniani FIFA limetangaza mwaliko rasmi wa timu hiyo kwenye michuano ya mabara kwa mwaka 2013.
Italia ilijitengezea mwaliko huo usiku wa jana baada ya kumuondoa mjerumani kwa idadi ya magoli mawili na kufanikiwa kuingia fainali itakayochezwa jumapili dhidi ya Hispania.
Katika michuano hiyo iliyoanzishwa na FIFA mwaka 1997 Italia in nafasi ya kukataa mwaliko kama ilivyowahi kufanywa  miaka  ya nyuma na nchi za ujerumani na Ufaransa.
Mabingwa mtetezi na mshiriki wa fainali ,Hispania tayari imekata tiketi ya kushiriki michuano itakayofanyika nchini Brazil kutokana na kuwa bingwa mtetezi wa kombe la dunia.