
Tiketi kwa
ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa (Oktoba 3 kwenye
uwanja wa taifa jijini Dar es salaam zitaanza kuuzwa kesho kwenye katika vituo
mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya
Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa moja kamili usiku.
Vituo vitakavyotumia kuuza tiketi hizo ni
Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom
Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala na Kituo
cha Mafuta Buguruni n ate=iketi zitaanza kuuzwa saa nne kamili asubuhi.
Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo
ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani , wakati shilingi 7,000 itakuwa kwa
viti vya Blue.
Lakini Sh. 10,000 ni kwa viti vya rangi
ya chungwa huku VIP C itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh.
20,000 na VIP A kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
Wakati huo huo, mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza ndiye atakayechezesha
mechi hiyo. Waamuzi wasaidizi ni Samuel Mpenzu kutoka Arusha na Efrony Ndissa
wa Dar es Salaam wakati mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment