Chama
cha waandishi wa habariza michezo nchini Taswa kimepokea nafasi ya mafunzo kwa
waandishi wa habari wanawake yaliyoandaliwa na kamati ya Olimpiki ya kimataifa
IOC, na muunganio wa kamati za Olimpik za Afrika ANOCA kupitia kamati ya
Olimpic Tanzania TOC.
Akizungumzia
hilo katibu wa Taswa Amir Muhando amesema mafunzo hayo yataanza kufanyika rasmi
Desemba 10 na 11 mwaka huu katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Amiri amesema TASWA imepewa nafasi za waandishi wa habari wanawake watatu washiriki kwenye mafunzo hayo na imepokea barua hiyo leo wakati siku ya Ijumaa ya wiki hii majina yawe yameshatumwa kwa wahusika.
baada ya kutolewa nafasi hizo chache Taswa imewataka waandishi wanawake wenye nia na muda wa kushiriki wawasilishe CV zao kabla ya Ijumaa (Novemba 2, 2012) saa sita mchana ofisini kwa Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (Hifadhi House ghorofa ya 9 zilipo ofisi za JamboLeo, Posta) au kwangu mimi ofisi za Daily News Tazara, Dar es Salaam.
Masharti ya mafunzo ni kuwa yataendeshwa kwa lugha ya Kingereza na Kifaransa, lakini pia watakaoshiriki wawe tayari kuja kutoa elimu watakayaoipata huko kwa wenzao pindi watakaporudi nchini.
Suala la CV ni la umuhimu kupita maelezo, kwani baada ya hapo mchana siku hiyo TASWA itateua majina matatu na kuyatuma TOC kwa taratibu nyingine.

0 comments:
Post a Comment