
Raisi wa SA,Jacob Zuma akiitaja Cape Verde kwenye kundi A.
Baada ya kukamilika kwa utaratibu wa upangaji wa makundi ya AFCON 2012, kule nchini Afrika ya kusini, washiriki wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza taifa la Cape Vede limetajwa kufungua michuano hiyo January 19, na wenyeji Afrika ya kusini.
Cape vede imepata nafasi hiyo adhimu baada ya kutajwa na raisi wa Afrika ya kusini Jacob Zuma katika hafla ya kupanga makundi iliyofanyika usiku wa jana jijini Durban nchini humo.
Katika makundi hayo, kundi A linawakilishwa na wenyeji Afrika ya kusini,Cape Verde, Morocco, na Angola, kundi B zipo timu za Ghana,DR Congo,Niger na Mali wakati kundi C linawakilishwa na timu za Zambia,Ethiopia, Nigeria, na Burkina faso.
Kwa upande wa kundi la mwisho kund ambalo linatazamwa kama la kwanza kwa ugumu linawakilishwa na Ivory Coast,Togo,Tunisia pamoja na Algeria.
Michuano ya AFCON ambayo kwa sasa taji lake linashikiliwa na timu ya taifa ya Zambia, kwa mwaka 2013 inatarajiwa kuanza rasmi January 19 mwakani na kumalizika February 10 mwakani kule nchini Afrika ya kusini.
0 comments:
Post a Comment