KABATI ACHANGIA KIKAPU IRINGA



            
Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya CCM Viti maalum Mh, Ritta Kabati ameahidi kuchangia kisi cha shilingi laki mbili za kitanzania kwaajili ua kuisaidia timu ya Basketi mkoa wa Iringa ili iweze kufanikisha safari yake ya jijini Tanga kwenye michuano ya Taifa cup kwa mwaka 2012.
Kabati amesema ni muhimu kwa viongozi wengine kujitolea kusaidia michezo kutokana na nafasi na faida kubwa inayopatikana kwenye michezo, huku akiongeza kuwa kuinua kikapu nyanda za juu kusini kunaleta faraja kubwa kwa mpaka sasa ni takribani miaka 15 Iringa haina cha kujivunia katika michezo takribani yote.
Naye makamu mwenyekiti wa muda wa shirikisho la kikapu mkoa Iringa IRBF amewataka wadau kuwa na imani katika kuchangia suala hilo kwa uongozi uliopo madarakani kwa muda huu umetengeza msisitozo wa hali ya juukatika kurejesha heshima ya mchezo wa kikapu mkoa humo.
Harambee ya hiyo ya kuchangia timu ya mkoa inaendelea IRBF kwa kushirikiana na kituo cha redio Ebony fm ya mkoani humo.

0 comments:

Post a Comment