TENGA KUICHA VODA IKUTANE NA YANGA.



        
                     Raisi wa TFF Leodga Tenga
Uongozi wa Shirikisho la soka nchini TFF, umesema kuwa suala la mgogoro wa nembo ya  mdhamni wanaliweka pembeni na kuwaachia wadhamini na vilabu husika wakae nakujadili suala hilo.

Raisi wa TFF  Leodga Chila Tenga amesema hayo hii leo katika Mkutano maalum na Waandishi wa Habari, uliofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam,amesema msimu uliopita Vodacom walimalizana na Yanga bila ya kuishirikisha TFF, katika mgogoro huo wa nembo.

Kuhusu uchaguzi Tenga amewataka wagombea kuwasilisha vielelezo vyenye sifa za kugombea na kusoma kanuni za uchaguzi ili kuondoa migogoro katika chaguzi mbalimbali za vyama vya soka.

Katika mkutano Tenga alimaliza kwa kusema kuwa uongozi wa Mpira ni wito na si kazi kama wanavyofikiri watu.

0 comments:

Post a Comment