
Armstrong enzi zake.
Mwanamichezo wa mbio za Baiskeli Lance
Armstrong anatakiwa kulipa pesa zote alizowahi kulipwa katika mataji yote saba
aliwahi kutwaa katika mashindano mbalimbali ya baiskeli.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa umoja
wa mashindano ya Baiskeli duniani UCI, Cristian Prudome siku moja baada ya bodi
ya mashindano hayo kumvua mataji saba ya Tua De Frens aliyowahi kutwaa.
Prudome amesema kanuni za mshindano
zinaeleweka kuwa mwana baiskeli yoyote akishindwa kufuzu katika kanuni zao
anapaswa kulipa mafungu yote alitwaa katika kipindi chake.
Inakadiriwa kuwa Amstrong alitwaa kiasi
cha paundi million 2.4 wakati kampuni ya bima ya Texas ikiwa tayari inamdai
kisi cha dola milioni 7 za kimarekani kama bonus aliyokuwa kipata kwenye
kampuni hiyo.
katika majuma mawili yaliyopita Amstrong alifungiwa maisha kujihusisha na mbio za Baiskeli baada ya kupatika hatia ya utumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu uliopatika kwa ushahidi wa kurasa zipatazo 1000.
Chanzo ni BBC.
0 comments:
Post a Comment