PARDEW ATAKA FA ITOE ADHABU KWA UNITED.



 
                   kocha wa Newcastle Alan Pardew.
Kocha wa klabu ya Newcastle United ya England Alan Pardew amesema chama cha soka nchini humo FA kinapaswa kumwadhibu mshambuliaji wa Manchester United Roben Van Persie baada ya kumpiga kiwiko cha makusudi kiungo Yohan Cabaye.
Tukio hilo lililotokea jana kwenye mchezo wa ligi kuu na United kushinda kwa magoli 3 kwa 0, Pardew amesema FA inapaswa kuchunguza vizuri tukio  hilo ambalo pengine mwamuzi Howard Webb hakuliona ndio maana hakutoa adhabu.
Kocha huyo amesema kitendo alichokifanya  Van Persie hakikuwa cha kistaarabu hivyo kwamujibu wa sheria za soka ni sharti aaidhibiwe.
Katika mchezo huo magoli ya Manchester United yamefungwa yalifungwa na John Evance,Patrice Evra na kiungo Tom Cleverly.

0 comments:

Post a Comment