MATOKEO YA MICHEZO YA LIGI KUU TANZANIA BARA.



Ligi kuu ya Tanzania bara iliendeleahapo jana kwa michezo minne kupigwa kwenye viwanja tofauti ambapo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, klabu ya soka ya Yanga iliibuka na ushindi wa magoli 3 kwa 0 dhidi ya vibonde wa ligi hiyo Polisi Morogoro.

Magoli ya Yanga yalifungwa na kinda wa timu hiyo Simon Msuva, Didier Kavumbagu na Hamisi Kiiza aliengia akitokea benchi.

Matokeo ya michezo mingine ni Azam FC hii leo ilishindwa kushika usukani wa ligi kuu bara baada ya kulazimishwa sare ya goli 1 kwa 1 na maafande wa Ruvu shooting.
Kule Manungu nako mambo yalikuwa magumu kwa Mtibwa Sugar baada ya kulazimishwa sare ya goli 1 kwa 1 na wakata miwa wenzao Kagera Sugar.

Kwa upande wa Coastal Union waliokuwa nyumbani kwao kule mkoani Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 dhidi ya African Lyon.
.................
Wakati huo huo, tukigeuza jicho katika ligi daraja kwa mwakilishi wa mkoa wa Iringa timu ya Kurugenzi ya Mufindi ilishindwa kutamba ikiwa nyumbani kwenye uwanja wa Wambi uliopo mjini Mafinga baada ya kufungwa goli 1 kwa 0 na Majimaji ya Songea.

Katika uwanja wa Jamhuri pale Morogoro timu ya Mbeya City iliibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 dhidi ya Burkinafaso huku goli Mbeya City likifungwa na Fidels Castor katika dakika ya 85 ya mchezo huo.

Hapo kesho kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro timu ya Polisi Iringa itacheza na Mkamba Rangers jioni ya leo katika kukamilisha ratiba ya raundi ya kwanza.

0 comments:

Post a Comment