
Cole akiwa na jezi ya England.
Mlinzi wa klabu ya Chelsea na timu ya
Taifa ya England Ashley Cole huenda ameingizwa kwenye adhabu na shirikisho la
soka nchini England kwa kosa la utovu wa nidhamu.
FA imemuingiza hatia Cole kutokana na kuandika
ujumbe wa kuthibisha kuwa aliongopa juu ya utetezi wa tuhuma ya Jonh Terry juu
ya ubaguzi wa rangi.
Chama cha soka nchini England FA
kimetoa siku tatu kutoka leo ikiwa na maana siku ya Alhamisi Cole awe
ameshajibu tuhuma hizo kabla ya mchezo wa kuwania tiketi ya kombe la dunia dhidi ya San Marino.
Kwa upande wake mshambuliaji wa zamani
wa Newcastle united Alan Shearer mwishoni mwa juma lililopita aliitaka FA
kumfungia nyota huyo haswa akose mchezo dhini ya San Marino huku akikumbushia
kufungiwa kwake baada ya kumkosea Nei Lenon mwaka 1998 katika mchezo wa ligi.
0 comments:
Post a Comment